Majeshi ya serikali ya Syria na wanamgambo ya Kikurdi yamepambana vikali na kundi la kigaidi la Daesh katika maeneo tofauti leo katika eneo muhimu karibu na mpaka na Iraq na Uturuki.
Majeshi tiifu kwa rais Bashar al-Assad na wapiganaji wa vikosi vya ulinzi wa umma vya Wakurdi YPG yamefanya mashambulizi makali dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh katika jimbo la kaskazini mashariki la Hasakeh.
Mkuu wa shirika linaloangalia haki za binadamu nchini Syria Rami Abdel Rahman ameliambia shirika la habari la AFP kwamba baada ya mapambano ya siku tatu , majeshi ya serikali yakisaidiwa na wapiganaji kutoka katika makabila ya Kirabu yamepata udhibiti wa vijiji 23 katikati ya jimbo hilo.
Amesema wapiganaji wa kundi la YPG pia wanapambana na kundi la kigaidi la Daesh katika makabila ya Waarabu nje ya kijiji cha Tal Tamr katika eneo la kusini magharibi ya jimbo la Hasakeh.